In Summary
  • Na tayari jina hilo lipo kwenye migongo yao pia baada ya Juventus kurudisha nusu ya Pauni 99 milioni walizotumia kuinasa saini yake kwa kuuza tu jezi ndani ya siku moja. Jezi 500,000 zenye namba na jina la Ronaldo zimeuzwa ndani ya siku moja tu.

CRISTIANO Ronaldo ni jina ambalo lipo kwenye mdomo wa kila mtu huko Italia.

Na tayari jina hilo lipo kwenye migongo yao pia baada ya Juventus kurudisha nusu ya Pauni 99 milioni walizotumia kuinasa saini yake kwa kuuza tu jezi ndani ya siku moja. Jezi 500,000 zenye namba na jina la Ronaldo zimeuzwa ndani ya siku moja tu.

Supastaa huyo wa Ureno, 33, analipwa mshahara wa Pauni 500,000 kwa wiki na mashabiki wa Juventus wanaonekana kufurahia kuwa na jezi zenye ‘Ronaldo 7’ ambazo zimeripotiwa kuuzwa kupitia tovuti yao. Ripoti zinafichua kwamba kila jezi moja inagharimu Pauni 92, hivyo karibu nusu ya pesa iliyolipwa kupata huduma yake imevunwa tu kwa muda mfupi.

Juventus imetangaza kwamba itamtambulisha staa huyo huko Turin kesho Jumatatu, siku moja baada ya fainali ya Kombe la Dunia ambayo itapigwa leo kati ya Ufaransa na Croatia. Ronaldo amefunga mabao 450 kwa miaka yake tisa aliyodumu Real Madrid.

ADVERTISEMENT