In Summary
  • Staa huyo anayelipwa mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki huko Arsenal, kwa sasa anauguza tu maumivu ya timu yake ya Ujerumani kuishia hatua ya makundi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia, huku zigo la lawama lote akibebeshwa yeye. Ozil amekuwa kwenye wakati mgumu kisa tu alipiga picha akiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kabla ya fainali hizo za Russia. Lawama zisizokoma zimemfanya Ozil akiri kwa kusema: “Dunia yangu imepinduka juu chini.”

MESUT Ozil ameambiwa hivi, asahau kabisa stresi zake za Kombe la Dunia na kwamba, atakaporudi Arsenal afahamu tu awe kwenye akili ya kazi.

Staa huyo anayelipwa mshahara wa Pauni 350,000 kwa wiki huko Arsenal, kwa sasa anauguza tu maumivu ya timu yake ya Ujerumani kuishia hatua ya makundi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 huko Russia, huku zigo la lawama lote akibebeshwa yeye. Ozil amekuwa kwenye wakati mgumu kisa tu alipiga picha akiwa na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kabla ya fainali hizo za Russia. Lawama zisizokoma zimemfanya Ozil akiri kwa kusema: “Dunia yangu imepinduka juu chini.”

Lakini, kocha mpya wa Arsenal, Emery amesisitiza kwamba Ozil anapaswa amalize matatizo yake huko kabla ya kurudi kwenye timu kwa sababu hakutakuwa na kisingizio kutoka kwa mchezaji ambaye analipwa mshahara mkubwa kuliko wengine. Ozil kwa sasa yupo kwenye mapumziko, lakini anatarajia kurejea kwenye kikosi cha Arsenal baadaye mwezi huu. Arsenal itakipiga na Man. City, Agosti 12.

ADVERTISEMENT