In Summary
  • Kwenye mechi hiyo, Emery hakutaka mchezo, ameshusha mziki wa maana, akimpa nafasi ya kucheza beki mpya, Sokratis, huku straika Pierre-Emerick Aubameyang akifanya yake baada ya kupiga ‘hat-trick’ kwenye mechi hiyo ndani ya dakika 15 tu.

UNAI Emery anatesti mitambo yake huko Arsenal na bahati mbaya imewalipukia Boreham Wood baada ya kuchapwa 8-0 na wababe hao wa Emirates katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na msimu mpya uliofanyika kwenye Uwanja wa Meadow Park.

Kwenye mechi hiyo, Emery hakutaka mchezo, ameshusha mziki wa maana, akimpa nafasi ya kucheza beki mpya, Sokratis, huku straika Pierre-Emerick Aubameyang akifanya yake baada ya kupiga ‘hat-trick’ kwenye mechi hiyo ndani ya dakika 15 tu.

Reiss Nelson akapiga la nne kabla ya Alexandre Lacazette kupiga la tano baada ya pasi nzuri ya Aubameyang. Baada ya mapumziko, Arsenal ilibadilisha wachezaji wote 11 na wale wapya waliongia wakaisaidia timu hiyo kufunga mabao matatu zaidi, kupitia kwa Eddie Nketiah, Henrikh Mkhitaryan na Jeff Reine-Adelaide. Wiki ijayo, Arsenal itakwenda Singapore ambako itacheza na Atletico Madrid na Paris Saint German.

ADVERTISEMENT