In Summary
  • Katika makala haya, JB aliweza kupiga stori na Mwanaspoti nakufunguka mambo mengi kuhusu kazi zake na maisha yake ya kawaida.

BAADA ya miaka 16 ya kuwapo katika fani ya sanaa ya maigizo, hakuna shaka kwamba, Steven Jacob maarufu kama JB, kwa sasa ni miongoni mwa watu wenye majina makubwa mno katika fani hiyo nchini.

Ni miongoni mwa nyota `Watano’ Bora zaidi wa kiume kwa upande wa fani hiyo, hivyo kumfanya kuwa katika hadhi ya juu, sawa na nyota wengine kama akina Vincent Kigosi `Ray’ Richie Richie na wengine.

 Ndiyo maana haishangazi kuona kwamba, hata leo hii ukiingia katika soko la filamu zilizo juu, huwezi kukosa kazi za nyota huyo.

Katika makala haya, JB aliweza kupiga stori na Mwanaspoti nakufunguka mambo mengi kuhusu kazi zake na maisha yake ya kawaida.

nizame kwenye tamthiliya na muvi niwaachie watu wengine.

Mwanaspoti:Habari yako Jacobo?

JB:Weee dada we,umeniita vizuru sana jina langu,nzuri na hongera

Mwanaspoti:Kwanini tena?

JB:Vyombo vya habari vingi vimezoea kuniita JB,sasa nimeshangaa sana kuniita jina langu halisi.

Mwanaspoti:Kuna habari zinadai kuwa,unapenda kutoka kimapenzi na wasanii wakike wa filamu. hilo lipoje?

JB:Yaani hili swali nishalijibu sana, ujue wale wasanii wa kike wananiponza sana,yaani wamenizoea sana na wengine kunifanya mimi kama babu yao,ila mapenzi hakuna kitu kama hicho.

Mwanaspoti:Vipi uliwahi kuchepuka?

JB: Aaah wapi weee namuheshimu sana mke wangu na sitaki kumkwaza na nichepuke ili iweje? Sijawahi kwakweli

Mwanaspoti: Unazungumzia vipi kuhusu adhabu ya Wema kupewa na Bodi ya Filamu ?

JB:Mie sina cha kuongea chochote hayo mambo ya Serikali wameamua.

Mwanaspoti: Kwa upande wako unalipi la kumshauri Wema Sepetu kuhusu video yake?

JB: Mimi binfsi sitaki kuzungumzia mambo hayo hadharani, nitaongea nae mwenyewe kwenye simu nikipata muda.

Mwanaspoti: Hivi Mpaka sasa kwenye muvi umefanikiwa kuvuna tuzo ngapi?

JB: Tuzo nyingi tu baadhi ni Mwaka 2008 nilipata Tuzo ya Muigizaji Bora kutoka Vinara Awards, 2011 nilipewa tuzo kama hiyo kutoka ZIFF (Zanzibar International Film Festival) kupitia muvi ya Simu ya Bachelor. Mwaka 2013, tuzo ya filamu bora kutoka Steps kupitia Muvi ya Shikamoo Mzee na Kipindi cha Action and Cut kimewahi kunipa tuzo kupitia muvi yangu ya Shikamoo Mzee.

Mwaspoti: Kutokana na ukongwe wako kwenye ‘game’ ya filamu mpaka sasa umecheza filamu ngapi?

JB: Sina takwimu sawasawa lakini zinachezea kwenye hamsini.

Mwanaspoti: Unajivunia pia kipi kwenye tasnia ya filamu?

JB: Kuonesha vitu vya tofauti na kukubalika zaidi. Lakini pia kuwaongezea vitu baadhi ya wasanii. Kwa mfano marehemu King Majuto alizoeleka kucheza muvi za vichekesho, lakini mimi nilimbadilisha na nikamchezesha muvi siriasi inayojulikana kwa jina la Nakwenda kwa Mzee.

Pia Wema Sepetu, Muvi ya DJ Ben ilimfanya kumpindua Irene Uwoya ambaye kipindi hicho ndiye alikuwa na jina zaidi kwenye tasnia ya muvi. Jackline Wolper naye Muvi ya Taxi Dreva ilimfanya kupanda chati zaidi, hivyo hivyo kwa Aunt Ezekiel Muvi ya Signature iliyojizolea mashabiki lukuki ambavyo sikutarajia kama itahiti.

Mwanaspoti:Asante sana

JB:Karibu tena

ADVERTISEMENT