NYOTA wa filamu nchini, Kajala Masanja amefichua kuwa, ishu za mimba shuleni hata yeye zinamgusa kwani, akiwa binti mdogo alipata ujauzito na kumtesa na ni matukio ambayo familia nyingi huwa ngumu kulikubali kwa urahisi.

Kajala alisema alinasa ujauzito akiwa kidato cha tatu na kukatishwa masomo, kitu ambacho amekuwa makini ili kuepuka binti yake kisimkute na pia kuielimisha

jamii juu ya madhara ya mimba za utotoni ili kuwanusuru watoto wa kike wakiwa shuleni.

“Nimeamua kuwa balozi wa kupinga mimba kwa wanafunzi au watoto wadogo kwa ujumla, kwani ni tukio hilo linaweza kuzima ndoto za binti yeyote, ambaye labda angekuja kuwa kiongozi au hata mtu mkubwa nchini, nimejitolea kuwaelimisha mabinti juu ya kujilinda na hila za wanaume,” alisema Kajala.

Alisema alishika ujauzito na kujifungua mwanae Paula na mtayarishaji maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, P Funky ‘Majani, japo kwa sasa imekuwa ni

mapito, ndio maana hataki kuona mabinti wanapita njia hiyo, kwani hakuna mzazi anayekubali bintiye akatishwe masomo ama ndoto zake za kimaisha.

ADVERTISEMENT