In Summary
  • Akizungumza na Mwanaspoti, Chemical amesema kuwa wasanii hasa wa kike hupitia mambo mengi ikiwamo kulazimishwa kutakiwa kimapenzi, lakini kwake ishu hizo hazipo.

SI unajua kuwa mastaa wa kike wamekuwa wakikumbwa na skendo kibao, lakini kwa staa wa Bongo Fleva, Cloudia Lubao a.k.a Chemical mambo ni tofauti na madume wanasanda.

Chemical anayetamba na ngoma ya ‘Nitajioa’, amefunguka kuwa wanaume wamekuwa wakiogopa kumsumbua kimapenzi kutokana na staili yake ya kujiweka kigumu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Chemical amesema kuwa wasanii hasa wa kike hupitia mambo mengi ikiwamo kulazimishwa kutakiwa kimapenzi, lakini kwake ishu hizo hazipo.

“Yaani huyo mwanaume akija kwangu lazima ajipange kwelikweli na awe na malengo, sio eti mtu anakuja kujaribu tu. Si unaona mwenyewe mikato yangu sasa lazima nimbane mtu,” alisema.

Alisema ni kutokana na hilo ndio sababu ya kuachia ngoma ya ‘Nitajioa’ ambayo, pamoja na mambo mengine inazungumzia wanawake wanaoishi maisha ya kigumu kama staili yake.

Hata hivyo, alisema kuwa licha ya jamii kuwachukulia tofauti kuwa hawawezi kuwa wake bora wa kuishi na wanaume, ukweli wanaweza kuolewa na wakawa wazuri ndani ya familia zao.

Kuhusu mipango ya kuwa na familia, Chemical alisema bado sana.

ADVERTISEMENT