In Summary
  • Biggie alisema ameigiza baadhi ya hadithi za vitabu kama Mfalme Juha, Idd Amin Dadaa na mingineyo jambo lililompa heshima kubwa ndani na nje ya nchi na kumshukuru mno mwongozaji wake Gonche Materego kwa kuona kipaji chake na kumtumia katika kila kazi anayoisimamia.

LUMOLE Matovolwa ‘Biggie’ amefunguka kwa kueleza kwa sasa ameamua kuwekeza nguvu kubwa katika uigizaji wa jukwaani badala ya uigizaji wa filamu baada ya kugundua inampa nafasi kubwa ya kutamba katika fani hiyo.

Alisema tangu amejitosa kwenye mfumo huo kila kitu kimekuwa muswano na anaamini atafika mbali zaidi na alivyo sasa.

“Awali nilikuwa nimewekeza katika uigizaji wa filamu tu na si michezo ambayo huwa mubashara (live) yaani kuigiza jukwaani kucheza tamthilia kutokana na vitabu mbalimbali, ila nikagundua anayeigiza jukwaani ana uwezo mkubwa.”

Biggie alisema ameigiza baadhi ya hadithi za vitabu kama Mfalme Juha, Idd Amin Dadaa na mingineyo jambo lililompa heshima kubwa ndani na nje ya nchi na kumshukuru mno mwongozaji wake Gonche Materego kwa kuona kipaji chake na kumtumia katika kila kazi anayoisimamia.

ADVERTISEMENT